ISLAMIC SOCIAL SOLIDARITY PROGRESSIVE
Monday, 3 October 2016
Saturday, 1 October 2016
ULIMWENGU WA KIISLAMU, FURSA NA CHANGAMOTO
Assalamu alaikum ndugu Waislamu
hichi ni kijitabu kilichokusanya idadi ya makala kutoka Radio ya
kiswahili ya Iran (kiswahili.irib.ir), na mkusanyaji wa makala hizi
ni ndugu yenu Salim Al-Rajihiy, kwa hiyo haki za kunukuu au kuchapisha
zimehifadhiwa na (kiswahili.irib.ir) Iran, na hakukua na malengo yeyote
katika kuzikusanya makala hizi, isipokua ni kueneza fikra na utamaduni
wa Kiislamu.
Ahsanteni sana tusiache kuombeana dua.
Mwaka Mpya Wa Kiislamu Na Hukumu Ya Kusherehekea
Mwaka Mpya Wa Kiislamu Na Hukumu Ya Kusherehekea
Tunaingia kwenye mwaka mpya wa Kiislam (Hijriyyah). Je, vipi tuukaribishe mwaka huu wetu mpya? Na nini hukumu ya kusherehekea? Na nini umuhimu wa miezi ya Kiislamu?
Kuhesabika Mwaka Mpya
Miaka yetu ya Kiislam imeanza kuhesabika baada ya Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba kuhajiri (Hijrah) kutoka Makkah kwenda Madiynah. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akatoa ushauri kuwa kwa vile ni mara ya kwanza wanahamia katika mji ambao wataanza kutekeleza shariy’ah ya Kiislam, basi ni bora kuanza kuhesabu ya miaka kwa kuanzia mwezi huo waliohajiri, ambao ulikuwa ni mwezi wa Muharram.
Na pia inasemekana kuwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu)
Wednesday, 24 August 2016
AL KAABA |
IBADA YA HIJJA
UMRA
Nini Hijja?
Hijja, kilugha ni kukusudia;
kisharia ni kukusudia kwenda Makka kutekeleza nguzo za Hija, tangu 'tawaf, sa'i
(Safa na Marwa), kuhudhuria 'Arafa, na nguzo nyengine za Hija. Hutenda haya
kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutafuta ridhaa zake.
Hukmu ya Hijja
Hija ni fardhi kwa kila mwenye
uwezo, ni nguzo ya tano miongoni mwa nguzo tano za Uislam. Hija imekuja kwa
Qauli ya wenyezi Mungu Mtukufu, qauli ya Mtume wetu Mpenzi s.a.w. na itifaqi ya
Umma. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"............Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea……". (Al 'Imraan : 97).
Na amesema Mtume wetu Mpenzi
s.a.w.:
"Umejengwa Uislam juu ya (Nguzo) tano", (mpaka mwisho wa Hadithi).
"Umejengwa Uislam juu ya (Nguzo) tano", (mpaka mwisho wa Hadithi).
Na amesema Mtume wetu Mpenzi
s.a.w.:
"Hijini kabla hamjakuwa hamuwezi kuhiji". (Imehadithiwa na Al Bayhaqy).
"Hijini kabla hamjakuwa hamuwezi kuhiji". (Imehadithiwa na Al Bayhaqy).
Mwenye kukanya kuwajibika Hija
huwa amekufuru.
Tuesday, 2 August 2016
TAASISI YA ISLAMIC SOCIAL SOLIDARITY PROGRESSIVE KWA KUSHIRIKIANA NA MEYA YA WILAYA YA TEMEKE WALIANDAA MASHINDANO YA QUR AN KATIKA KIPINDI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI MASHINDANO HAYO YALIHUSISHA WASHIRIKI WA JUZUU 3,5,7, PAMOJA NA JUZUU KUMI ZAWADI MBALIMBALI ZILITOLEWA KWA WASHINDI WA KWANZA ,PILI NA WATATU KATIKA KILA KUNDI
ZIFUATAZO NI VIDEO ZA BAADHI YA WASHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO
ZIFUATAZO NI VIDEO ZA BAADHI YA WASHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO
YA PILI
Friday, 17 April 2015
Friday, 3 April 2015
madhara ya bidaa katika uislamu
BIDAA NA VIPENGELE VYAKE
Baadhi ya vipengele vya Bid’ah ni kama vifuatavyo:
1. Kila bid’ah ni Dhwalaalah.
Kilugha
Bid’ah ni kitu chochote kipya au kitu ambacho hakijafanywa kabla,
yaani, hakina mfano kabisa wa mbeleni. Katika muono wa kisheria, kila
Bid’ah ni Dhwalaalah na hakuna Bid’ah hasanah au sayyi’ah (Bid’ah nzuri
na mbaya). Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema
katika hadith, “Kullu Bid’atin dhwalaalah wa kullu dhwalaalatin fin naar (kila Bid’ah ni Dhwalaalah na kila Dhwalaalah ni motoni)” (Imepokewa na Imam Ahmad, Abu Dawud, at-Tirmidhy na wengineo).
Dhalalah
ina maana ya kwenda kombo au kufuata njia ya upotevu na kwenda kinyume
na ukweli. Tukitazama Qur-aan, tutaona vipi Allaah (Subhaanahu Wa
Ta'ala) ametumia neno hilo
‘dhwalaalah’ au ‘dhwaal’. Neno hili linatumika kwa mtu anayefanya
dhambi au anafanya kosa katika mambo ya kidini lakini na pia linatumika
kwa wale watu ambao wamepotea kutoka kwa njia nyoofu au wale walioigawa
dini. Kwa mfano katika Suratu Faatihah (Sura ya kwanza), neno
lililotumika ni ‘Dhaaliin’ halikutumika kwa wafanyao madhambi pekee
lakini limetumika kwa watu waliopotea kutoka kwa ile njia ya sawa, yaani
Wakristo. Hivyo pale Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
alipoielezea bid’ah, alitumia neno kali sana kwa upotevu huo, yaani dhalalah, kama alivyosema, “Kulla bid’atin dhwalaalah (kila bi’dah ni dhwalaalah)”. Hakusema kuwa kila bid’ah ni dhambi au ni kosa lakini kwa hakika ni jambo ambalo ni kubwa kuliko hilo. Huu ni upotevu, jambo ambalo linamtoa mtu katika Swiraatul Mustaqiym (njia ilinyooka).
Subscribe to:
Posts (Atom)