historia ya mitume

HISTORIA YA MAISHA YA MITUME

Bismillah Ar-rahmaan Ar-rahiim.

HISTORIA YA NABII ADAM (A.S)


Allah (S.W) kitu cha kwanza kukiumba ulimwenguni ni Qalam ambayoameiumba kwa ajili ya kuandika mema na maovu ya viumbe, aliumba Lauhul-Mahfuudhna vyenginevyo. Allah aliumba mbingu saba (7) siku sita (6) katika matabakambali mbali pamoja na mchanga (ardhi) siku ya Jumaamosi, aliumba majabalikatika siku ya Jumaapili, miti siku ya Jumaatatu, vitu vyote vyenye kuchukizaaliviumba Allah katika siku ya Jumaane, nuru siku ya Jumaatano, viumbe katikasiku ya Alhamis na mwisho alimuumba Adam (AS) katika siku ya Ijumaa nyakati zaAlaasiri ndio siku ya mwisho ambayo wanaadamu wote wataondoka ulimwenguni.

Lakini kabla ya kuumbwa Nabii Adam, Allah alikuwa tayariamekwishawaumba majini ambao walifanya ufisadi katika ardhi na walimwaga damuza wengine. Hatimae Allah aliwapelekea majini hao jeshi la malaika nawakateketezwa majini wote. Mara tu baada ya Allah kuwateketeza majini hao, malaikaJibriil alimbakisha mmoja katika kizazi cha majini aliyeitwa AZAAZIIL (Iblis)kwa vile jinni huyo alimuabudu sana Allah, hivyo Allah alimuweka pamoja namalaika peponi. Iblis aliendelea kumwabudu Allah mpaka akafikia kuitwaAbaasijda, kutokana na wingi wa sijda zake kumsujudia Allah. Hivyo ijapokuwahakuumbwa kwa nuru (aliumbwa kwa moto),  lakini Iblis alishirikiana na malaika katikaibada kumwabudia Allah.

Siku moja Allah aliwadokeza malaika kuwa anataka kuumba kiumbemwengine duniani. Malaika wakafikiri mambo yaliyowatokea kabla ya Adam, najinsi wale majini walivyofanya ufisadi katika ardhi.
Hivyo malaika hao wakasema kwa kumuuliza katika quran tukufu,“Ewe molaunataka kuweka katika ardhi anaetaka kufanya ufisadi na kumwaga damu, kamawalivyomwaga damu waliopita. Au unataka kuleta kiumbe atakaekuabudu kwa wingina je! Sisi tumepunguza kitu katika ibada yako? Na hali sisi tunakutukuza natunakusabbihi kila usiku na mchana?”.
Nae Allah akawaambia katika qurani tukufu, “Mimi ninajuwa vilemsivyovijuwa nyinyi”.
Kutokana na uchamungu wao malaika wakasema ,”Basi aumbe Allah vileanavyovipenda katika viumbe. Lakini hawatokua viumbe hao wabora na wajuzi kulikosisi”.

Hivyo Allah akauchukuwa mchanga wa aina mbali mbali na akaufinyangakwa hatua mbali mbali mpaka ukafikia kwenye kiumbe mfano wa sanamu. Hivyo Allahakasimamisha sanamu hiyo ya Adam kwa muda wa siku arubaini (40), na wakatiikiwa imesimama kila siku malaika walikuwa wakipita na kuiangalia sanamu hiyoiliyoweka uwanjani hapo. Hivyo hapo sasa ikawa ni mwanzo wa fitna na kejeli kwaiblis kwani alihisi kiumbe huyo atakuja kupewa thamani kubwa kuliko wao, lakinimmoja wa malaika alipewa elimu ya kujuwa kitu cha baadae na Allah hivyo akawaanawatoa wasiwasi wenzake juu yakiumbe hicho.

Katika siku ya arubaini Allah akaileta roho na kuanza kukipuliziakiwiliwili hicho. Hapo Adam akapiga chafya na ndipo malaika wakamwambia Adam, “EweAdam sema alhamdulillahi kwani roho ndio kwanza imewasili”. Adam hapo hapo kwakushkuru akasema alhamdulallahi na Allah akamuitikia na ndipo roho ikaingiamachoni ambapo Adam akaona matunda ya aina kwa aina peponi. Akaanza kuyatamanimatunda yale ilhali roho haijafika hata tumboni, akataka pia kutembea wakatiroho haijafika hata miguuni, na ndio maana mwanaadamu akawa ana tabia ya kuwana pupa katika mambo yake siku zote. Roho taratibu ikaingia kiungo kimoja baadaya chrengine mpaka ikamalizia miguuni. Hapo ndipo Allah akamuamrisha Adam apitembele ya malaika na awatolee salam na hapo ikawa ni mwanzo wa salam katikaUislam. Allah akasema, “Haya yatakuwa ni maamkizi kwa umma wako”.

Allah alimfundisha Adam majina ya vitu vyote duniani, pamoja na matumiziya vitu hivyo. Allah alivileta vitu hivyo mbele ya malaika naakawaambia,”Nielezeni majina ya vitu hivyo ikiwa nyinyi ni wakweli”. Malaikawakashindwa na wakajibu kumwambia Allah,”Utakasifu ni wako ewe mola, na sisihatuvijui vitu hivyo ispokuwa vile ulivyotufundisha tu”. Allah akamleta Adam naakamwambia avitaje vitu hivyo vyote, nae Adam hakusita akavitaja vitu hivyovyote. Hapo ndipo Allah akawaambia malaika, “Ninayajuwa yale msiyoyajuwa, basimsujudieni Adam”. Hapo malaika wote walisujudu ispokuwa Iblisi pekee akakataana akafanya kiburi na akawa ni miongoni mwa waliokufuru. Allah akamuulizaIblisi, “Ni kipi kilichokuzuia kumsujudia Adam pale nilipokuamrisha?”. Iblisiakajibu,”Mimi ni bora kuliko yeye umeniumba kwa moto naye umemuumba kwaudongo”. Hapo ndipo Allah akamjibu,”Toka katika rehma zangu, huna uwezo wakukataa amri yangu. Basi utakuwa ni miongoni mwa madhalili”. Iblisi akasema kwaAllah,” Ewe mola umenilaani kwa sababu ya kutomsujudia kiumbe hichi. Nipe mudaniishi”. Allah akamkubalia ombi lake kwa kusema,”Utaishi mpaka mwisho waulimwengu”. Iblisi akasema,”Hakika nitawazuia waja wako katika kukuabudu nanitajitahidi. Hivyo hutowapata wengi wao walionusurika”. Allah akamjibu,”Basiondoka hali ya kuwa ni dhalil na yeyote atakaekufuata nyote mtakuwa motoni”.

Adam aliishi peponi pekee hali yakuwa ni mpweke, na Allah alimuonaAdam akiwa ni mynonge peponi akiranda huku na kule bila ya mtu wa kumliwaza.Hivyo siku moja Adam alihisi maumivu makali ubavuni mwake kushoto, kumbe Allahalikuwa anamtowa kiumbe mwengine katika mwili wake kutokana na yeye. Adamalipoteza fahamu na mara tu baada ya kushtuka alikuta kiumbe kimemsimamia.Malaika ambao walikuwa karibu wakataka kumpa mtihani Adam kama ni kwelianafahamu kila kilchomo ulimwenguni, wakasema kumuuliza,”Ewe Adam ni nanihuyo?”. Adam akawajibu, “Huyu ni utulivu kwangu”. Malaika wakamuuliza tena,”Je!Unamjuwa jina lake?” Adam akajibu,”Jina lake ni Hawaa”. Hawaa ni jina lenyemaana ya ubavuni na alikuwa ni mwanamke mzuri zaidi duniani kuliko wanawake wote.Hapo ndipo malaika wakamuuliza tena Adam,”Kwa nini ameitwa Hawa?” Adamakawajibu,”Kwa sababu ametokana na kiumbe hai”.

Allah akamwambia Adam,”Ewe Adam ishi na mkeo peponi na kuleni kilakitu ispokuwa kimoja tu msikikaribie (mti). Kwani mtakuwa ni miongoni mwamadhalimu.” Maisha ya Adam na Hawa yalikuwa ni mazuri tu peponi kwa vilewalistarehe kwa kupata kila kitu walichokihitaji, na wakawa na hadhari kubwasana kwa kufuata waliyoamrisha na kujiepusha na waliyokatazwa. Kilawalipoukaribia ule mti haraka walijiweka mbali nao, matunda yake hayakuwa nimazuri kama yalivyokuwa matunda mengine na Allah aliwakataza tu ili kuwapamtihani. Iblisi aliumia na kuwaonea choyo na alikuwa Adam ndiye aliyesababishakutolewa kwake katika rehma za Allah peponi. Hapo Iblisi akaanza kuwaza jinsiya kuwafanya Adam na Hawa wamuasi Allah ili nao wafukuzwe katika neema hizo.Mwishowe akaona awafanye wavunje lile sharti walilopewa na Allah yaani wakalalile tunda la ule mti uliokatazwa. Iblisi aliona kuwa wanapendana sana na akatumiamapenzi yao kuwaondosha peponi, akaanza kujirusha rusha na kupiga ngoma nakufurahi kwa vile aliona njia hii ni sahihi. Hivyo Iblis akaanza kujiwekamahala ambapo Adam na Hawa watamouna na bila ya wao kumtambuwa kama ni Yulealiyefukuzwa peponi. Akawa analia sana na ndipo Adam na Hawa walipomshangaakumwona mtu analia katika eneo hilo, hapo hapo wakamsogelea na kumuuliza. Iblisakawajibu, “Nakulilieni nyinyi.” Adam akamuuliza huku akimsogelea,” Ki vipi?”.Iblis aliendelea,”Kwa sababu mtakufa na kuziwacha nyuma neema zote mlizonazo.”

Ghafla Adam na Hawa wakaingia huzuni, ndipo Iblis alipoona kuwaameshawaweza kwa namna ya kwanza ya kuwatia huzuni. Adam na Hawa hawakumjuwaIblis kwa taswira aliyoyojifananisha. Juu ya yote hayo Allah alishawaambia kuwawatakaa humo milele, lakini Iblis akawashawishi na kuwapa fikra nyengine kuwawatakufa na wataiacha pepo. Hawa alivutwa ziadi na Iblis na akawaanamhakikishia Adam ya kuwa neema zao hizo zitawatoka, lakini Adam alikaza moyona akaamuwa aachane na mawazo hayo. Pia Adam moyoni mwake akawa na hofu juu yamaneno hayo, na ndipo wakawa hawana tena furaha wakati wlipokuwa wakitembeapeponi. Siku chache mbele walikutana tena na Iblis, Iblis akawauliza, “Je!Mumefikiria jambo ambalo litakufanyeni make milele humu peponi?” Kwa pupa Hawaakamuuliza, “ Ni jambo gani hilo na inawezekanaje?”. Iblis alijifanya anajuwazaidi ukweli wa mambo na ndipo akamgeukia Adam na kumwambia, “Ewe Adamnikujuulishe mti utakaokufanyeni make milele?” Wote wakaitikia na Iblisakaendelea kusema, “Kuleni matunda ya mti ulee (mti uliokatazwa).” Adam akajibukwa mshangao, “Lakini sisi tumeshakatazwa na mola wetu.”Mola wenuhajakukatazeni ila msijekuwa nyinyi malaika au kuwa wenye kukaa milele.” Iblisakawapia kwa kusema, “Hakika mimi kwenu ni mtoaji nasaha mzuri hivyo msijemkakataa na mkajuta”.

 Hivyo Adam akawa tayari kulatunda la mti huo na alishawishiwa zaidi na mkewe Haw, ingawa hapo awali alikuwani mpinzani mkuu. Sauti ya mwanamke ilimhadaa na hapo hapo walikula matundayale wote wawili. Mara tu walipokula nguo zao zikawavuka na ikadhihirika aibuyao iliyokuwa imefichwa na wakawa uchi huku wakitafuta majani ya humo peponiili wajifunike tupu zao. Adam akamuasi mola wake na Iblis akatimiza kwa mara yakwanza lengo lake (Suratu ttwaaha). Allah akawaita, “Ewe Adam, ewe Hawa! Je!Mimi sikukukatazeni kuwa msile matunda ya mti huu? Na nimekwambieni mbele kuwashetani ni adui aliye wa wazi kwenu?” Wote wawili wakasema kwa majuto,” Ewemola wetu hakika sisi tumejudhulumu wenyewe nafsi zetu, na usipotusamehe nakuturehemu tutakuwa ni miongoni mwa waliokula hasara”. Adam akaanza kukimbiapeponi kwa haya ya kumwogopa mola wake. Allah akamwambia, “Ewe Adam leo hiiunanikimbia?” Adam akajibu, “Ewe mola wangu, nakimbia kwa sababu ya kuonahaya.” Allah akamwambia, “Shukeni huko peponi kwani baadhi yenu na baadhi yawengine ni maadui, nendeni katika ardhi.”

Wote wakatereshwa ardhini na kila mmoja akateremshwa sehemu tafauti namwenzake. Adam aliteremshwa India na Hawa aliteremshwa sehemu iitwayo Jidaa(Khaleej Mamlakatu – Aaraabiyyah) na Iblis akateremshwa Baabiil. Hawa akaanzakumtafuta Adam na Adam nae akaanza kumtafuta Hawa. Hivyo wote wakaanzakuhangaika na uzito wa maisha ukaanza, kama alivyokwishaambiwa na Allah kuwa atapatashida. Baada ya mahangaiko marefu wote wawili wakakutana sehemu iitwayo Arafah(Wanazuoni wamepaita jina hilo kwa sababu ya kujuana kwa Adam na Hawa). Hivileo ni sehemu amabayo hukutana mahujjaj ndani ya mfunguo tatu (30) mwezi tisa(9). Hivyo katika sehemu hiyo Adam na Hawa wakaanza maisha mapya.

Huku awali Allah aliwaambia, “Shukeni huko huko iwapo utakujieniuongofu. Basi mwenye kufuata uongofu wangu hatopotea wala hatokuwa mbaya.Lakini Yule atakaeupa mgongo utajo (uongofu) wangu, basi ajuwe kuwa atakuwa namaisha ya dhiki na tutamfufua siku ya kiama hali ya kuwa ni kipofu. Atauliza :Ewe mola wangu mbona umenifufuwa kipofu. Allah atamjibu : Wewe ulizipuuza ayazetu...”

HABIL NA KABIL :
-Kuanza kwa ndoa-
Mara tu baada ya kukutana Allah akawapa kizazi wote wawili. Allahakawajuulisha jinsi ya kupata watoto, na wakaingiliana mpaka ikaja ishara kuwaHawa atapata motto wa kwanza aliyeitwa Kabil na dada yake, na mwengine ni Habilna dada yake mpaka watoto wote wakafika arubaini (40). Kila mimba iayozaliwailikuwa ni pacha (wa kike na kiume). Wakwanza aliitwa Habil na wa mwishoaliitwa Abdul- Mughiir na dada yake. Kizazi kiaenea kidogo kidogo na watotowakawa na ndugu kila mmoja na pacha wake. Kabil kazi yake ilikuwa ni kulima naHabil alifuga wanyama na Adam alifanya shughuli zake za kawaida na maishayaliendelea vizuri tu.

Watoto wakawa ni watu wazima na walihitaji kuoa. Lakini ikatoka sheriakutoka kwa baba yao Adam ambae ni mtume wao kuwa kila mmoja ikiwa anatakautulivu basi aoe pacha wa mwenzake. Hivyo ikawa Habil anatakiwa amuoe pacha waKabil na Kabil amuoe pacha wa Habil. Hivyo hapo ugomvi ukaanza ya kuwaitakuwaje Kabil amuoe pacha wa Habil ilihali pacha wa Habil si mzuri, Kabilalitaka amuoe pacha wake mwenyewe. Adam akamwambia Kabil , ‘’Haiwezekani wewehuyu ni dada yako, huwezi kumuoa, muoe yule kwani ndivyo ruhsa ilivyotolewa’’.
Kabil alikataa na Adamu akamwachia Allah (S.W) mwenyewe apitishe hukmubaina yao. Kabil akachukuwa nafaka na Habil akapeleka kondoo mnene katikauwanja wa hukumu. Hapo ndipo Allah (S.W) akapeleka umeme ambao ulimchukuwakondoo wa Habil, kuonesha kwamba Habil amekubalika mbele ya Allah (S.W) amuoepacha wa Kabil, na nafaka zikaachwa pale pale kuashiria ya kwamba hakukukubalikaamuoe pacha wake mwenyewe.

-Kifo Cha Habil-
Hivyo Kabil alipoona Habil amekubaliwa akamwambia:
‘’Madam Mungu amekukubalia wewe, basi nitakuuwa’’.
Habil akamjibu: ‘’Mimi nimekubaliwa kwa kuwa ni mchamungu, naweukinyanyuwa mkono wako kuniua mimi sitokufanya lolote nitamuachia Mungu kwaninamuogopa Allah (S.W)’’.
Hapo hapo Kabil akafanya njama za kumuua na Iblisi akamfundisha kwakumwambia: ‘’Wewe unataka kummaliza huyo? Basi mnyatie kalala, mpige jiwaatakufa’’ (Kwa mujibu wa wanazuoni). Basi akatumia njia hiyo na akamuua naakawa ni miongoni mwa wale waliokula khasara.

Kwani Mtume (S.A.W) anasema : ‘’Jiepusheni na madhambi saba (7) yenyekuangamiza...’’ Ambapo miongoni mwao ni kuuwa. Baada ya hapo Kabil akambebandugu yake Habil mgongoni na akawa hajui cha kufanya kwa vile alimuona tayariameshakufa. Habil alikuwa ni mwenye nguvu kuliko Kabil lakini alimuachiaamdhuru kwa vile Habil alikuwa ni mstaarabu na mchamungu. Kama Mtume (S.A.W)anavyosema kuwa ukakamavu si kuwa maguvu mengi, lakini ukakamavu (hodari) niyule ambae anaimiliki nafsi yake wakati wa ghadhabu. Hivyo mpaka hii leo mtuakiuwa kwa makusudi duniani, Kabil anapata adhabu kaburini kwa vile yeye ndiyewa kwanza kuanzisha njia hii mbaya.

Allah (S.W) alipomuona Kabil anahangaika akampelekea kunguru wawili.Kunguru hao wakapigana mpaka mmoja wao akamuuwa mwenzake. Baada ya kumuuwaakachimba shimo ardhini na alipomaliza akambeba mwenzake na kumfukia shimonihumo. Kabil baada ya kuona tukio hilo naye akasema :’’Kwa nini nami nisichimbeshimo ili niifukie maiti ya ndugu yangu.’’ Hapo hapo nae akamzika ndugu yakeHabil na akawa ni mwenye kujuta. Adam (A.S) baada ya kusikia habari za kifohicho akahuzunika huzuni kubwa sana ya kifo cha Habil. Allah (S.W) anasema :
‘’Kwa ajili ya hayo tuliwaambia Banuu-Israiil kwa yoyote atakayeuwanafsi kwa dhulma ni sawa na kumwaga damu ya viumbe vyote’’.
Mtume (S.A.W) pia anasema :’’Mwenye kuuwa akashiriki japo kwa nusuneno, anaandikwa katika kipaji chake cha uso kuwa amekata tama na rehma zaAllah (S.W)’’.

-Maradhi na Kifo Cha Adam (A.S)-
Adam (A.S) alimlaumu Kabil na tokea hapo akaishi umri wake mrefu tumpaka siku moja alipopata maradhi kitandani. Aliwaita watoto wake na kuwaambia:’’Enyi wanangu nina hamu ya kula tunda la peponi, hebu nendeni mkanitafutie’’.
Watoto wakatoka kwenda kumtafutia baba yao tunda la peponi, na kamailivyo ada ya mtu anaekaribia kufa hutamani vitu vingi tu pengine vyenginehaviwezekani kupatikana kwa wakati huo. Njiani wakakutana na malaika Jibriilnae akawauliza, ‘’Mnakwenda wapi?’’. Watoto wakamjibu, ‘’Tunakwenda kumtafutiababa yetu tunda la peponi. Malaika akawaambia, ‘’Rudini kwani baba yenuameshakufa’’.

Waliporudi wakamkuta baba yao kweli ameshakufa, lakini Adam (A.S)alishawaahidi kuwa yeye na watoto wake watarudi peponi baada ya kufa kwakutenda mambo mema. Pia Bi Hawa hakuwa na hali nzuri na hivyo ulipofika mudamalaika wakafika tayari kwa kuichukuwa roho yake. Hapa wanazuoni wanasema kuwamalaika wenyewe wakamtia sanda, wakamsalia kwa takbira nne (4) na wakamchimbiakaburi na kuwaambia watoto wake kwamba, ‘’ Hii itakuwa ndiyo sunna yenu navizazi vyenu’’.

Wanazuoni wengi walitofautiana kuhusu sehemu aliyozikwa Adam (A.S),yaani husema kuwa alizikwa India, wengine husema alizikwa jabali maarufu yaaniJabal Abiy Qubays pale Maka, wengine husema alizikwa Baitul Maqdis, ilhalimiaka michache tu baada ya kifo cha Adam (A.S) alikufa Bi Hawa. Kizazi cha Adamkikawa na dini ile ile ya Uislamu na sheria zile zile za Adam (A.S) nahawakuabudia masanamu. Mtoto maarufu aliyepatikana katika zama hizo alikuwa niShiif ambae alikuwa ni nabii na kupewa suhuf (kurasa) baada ya Adam (A.S)ambapo nae pia aliendeleza daawa na kalmia yake ilikuwa ni: Muabuduni Allah(S.A) na jiepusheni na ibada ya masanamu. Hivyo umma huu mpaka kufikia kwaNabii Nuhu (A.S) ulikuwa ni mmoja na haukuwa na mabadiliko yoyote, walimfuataMungu mmoja na ibada ya masanamu ilikuwa ni mwiko

MWISHO

2 comments:

  1. assalamu alaikum me naomba kuuliza swali kama mtu itatokea katika swala amerukuu kabla ya imamu kurukuu lakini kwa kusahau hapo hukumu yake ipoje naomba mnisaidie

    ReplyDelete
    Replies
    1. hapo hana tatizo swala yake itakuwepo ila anatakiwa kua makini kimawazo katika swala kwani mtu hulipwa swala yake kutokana na kule kuwa kwake hadhiri katika swala

      Delete

add your comment here